Tuesday, August 20, 2013

WAKAZI WA KIGOMA WALIPOKEA KWA KISHINDO TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013

Shilole na madansa wake wakiwachengua vilivyo wakazi wa Kigoma,waliojitokeza kwa wingi  kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia kwenye jukwaa la tamasha la Serengeti Fiesta 2013, kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.

 Burudani ya kutosha kabisa

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cassim Mganga akiimba jukwaani mbele ya maelfu ya wakazi wa Kigoma ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.

 Msaniii anekuja kwa kasi kwenye miondoko ya Hip Hop,Stamina akikamua jukwaani mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Kigoma waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta
 Ni Shangwe tu ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rachael kutoka THT,akionesha umahiri wake wa kutumbuiza jukwaani usiku kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Washabiki wa tamasha la Fiesta wakifuatilia kwa makini yanayojiri  ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Wadau nao wamejitokeza kwa wingi
Peter Msechu na densa wake wakikamua vilivyo usiku kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.

TAMASHA LA KILI MUSIC TOUR 2013 JIJINI MWANZA


Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya (Bongo Fleva),Nassib Abdul a.k.a Diamond akiwajibika jukwaani sambamba na madansa wake wakati wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza na mikoa ya Jirani waliokataa kupitwa na Onyesho hilo kabambe. 
Diamond akiwa amenyanyuliwa juu na madansa wake wakati wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza

Mkali wa Ryms afahamikae kama Joseph Haule au ukipenda waweza muita Profesa Jay wa Mitulinga akiwapagawisha vilivyo wakazi wa Jiji la Mwanza waliofurika kwa wingi ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba kwenye Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza

Wanamuziki wakongwe katika medani ya muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydee na Joseph Haule au ukipenda waweza muita Profesa Jay wakiburudisha maelfu ya mashabiki wa muziki waliofurika katika Uiwanja wa Ushirika mjini Moshi mwishoni mwa wiki katika muendelezo wa Maonyesho ya Tamasha la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013. 
Mwanadada nguli katika tasnia ya Muziki hapa nchini,Muite Bint Komando au Lady Jaydee akifanya vitu vyake ndani ya jukwaa moja la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Wakongwe katika medani ya muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydee na Joseph Haule a.k.a Profesa Jay wakionyesha uhodari wao kwa kulishambulia jukwaa mbele ya maelfu ya mashabiki wa muziki waliofurika kwa wingi katika Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Mwanamuziki bora wa Hip Hop hapa nchini kwa mwaka 2013, Kala Jeremiah akiwarusha mashabiki wake waliofurika kwa wingi katika Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Kala Jeremiah akiendelea kufanya vitu vyake jukwaani.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Msanii Bob Junior akiimba moja ya nyimbo zake wakati wa muendelezo wa awamu ya pili ya Onyesho la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Bob Junior na madansa wake.

Mkali wa Miondoko ya Miduara,AT akiwapagawisha mashabiki wake lukuki ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Mkali wa RnB,Ben Pol akifanya vitu vyake jukwaani.
Roma Mkatoliki akifanya mambo yake jukwaani.
Shangwe tupu zilitawala uwanjani hao.
Ngoooshaaa....... Ngoooshaaaa....Ngooooshaaaaaa....... au ukipenda waweza muita Fareed Kubanda kwa jina alilopewa na Wazazi wake na pia waweza muita Fid Q akikamua vilivyo ndani ya Uwanja wa nyumbani huku shangwe zikitawala uwanjani hapo.
Fid Q na kamuzi lake likiendelea.
Mkali wa miondoko ya Ragger, Dabo akipigwa tafu na msanii mwenzake,Had Man
Snura Mushi a.k.a Mamaa wa Majanga akionesha umahiri wake mbele ya mashabiki wake wa jiji la Mwanza waliofurika kwa wingi katika Uwanja wa CCM Kirumba,jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, kushuhudia onyesho la Tamasha la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.

USAILI WA KUTAFUTA MODELS WATAKAOSHIRIKI KWENYE ALLY REHMTULLAH 2014 COLLECTION FASHION SHOW WAFANYIKA JIJINI DAR


DSC_0037 

Meza kuu ya Majaji walioshiriki katika Usaili ya kutafuta Models watakaoshiriki kwenye Ally Rehmtullah 2014 Collection Fashion show kutoka kushoto ni Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja, Ally Hassan, Mrembo na mwigizaji maarufu nchini Wema Sepetu, Mwandaaji wa Onyesho hilo ambaye pia ni Mbunifu wa Mavazi nchini Ally Rehmtullah, Mwanamitindo Jamillah Nyangasa, Sarah Raqey.


DSC_0050   
Pichani juu na chini ni Models wa kike wakipita mbele ya majaji wakati wa Audition ya kutafuta washiriki watakaonyesha mavazi kwenye Onyesho la Mavazi la Ally Rehmtullah 2014 Collection.
DSC_0049
DSC_0053
DSC_0082
Pichani juu na chini ni Models wa kiume wakipita mbele ya majaji kwa ajili ya kuchaguliwa kushiriki kwenye Ally Rehmtullah 2014 Collection Fashion Show.
DSC_0080
DSC_0069
DSC_0071