Tuesday, April 7, 2015

CHRISTIAN BELLA kukinukisha April 18 ndani ya ESCAPE ONE


bella
MWANAMUZIKI Christian Bella anatarajia kufanya shoo kubwa aliyoipa jina la Usiku wa Masauti, Aprili 18 Mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Escape One, uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
bella2
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Bella alisema katika usiku huo, pia atatambulisha video na audio ya wimbo wake mpya uitwao Nashindwa ambao tayari upo hewani.
bella3
“Natarajia kufanya shoo kubwa ambayo itanipa fursa ya kuwakutanisha wasanii wenzangu ambao wana nia safi ya kufanya mapinduzi kwenye muziki wetu wa dansi unaodaiwa kupotea, binafsi ninaumia sana ndiyo maana nimetumia kiasi cha dola 10,000 za Marekani kwa ajili ya kutengeneza video hii, naamini nitakuwa wa kwanza kwa kazi bora kama hii na ninaomba wenzangu waniunge mkono.”
bella6
Katika shoo hiyo, Bella amesema atasindikizwa na THT Band, Malaika Band pamoja na msanii kutoka nje ya nchi aitwaye Alice ambaye tayari ameshathibitisha kuunguna naye kwenye shoo hiyo na itakuwa mara ya kwanza kwake kuja Tanzania na kufanya shoo kubwa.
bella7
“Naomba mashabiki waje kwa wingi ili waone ni jinsi gani ninavyopigana kuweka maboresho katika dansi, huku nikiamini kabisa muziki huu ni moja ya burudani inayopendwa na watu wengi hapa Tanzania na ndiyo maana hata video ya wimbo wangu nimeifanya kimataifa zaidi ili kubadili ladha na mazoea ya muziki wetu,” alisema Bella.
SOURCE: http://www.cloudsfm.co

ALI KIBA AFUNIKA SHOO YA MWANA DAR LIVE

Mwanamuziki Ali Kiba akizikonga nyoyo za mashabiki waliofurika Dar Live katika shoo yake ya Mwana Dar Live iliyokuwa ikipigwa kwa ‘Live Band’.
Ali Kiba na mdogo wake Abdul Kiba wakichekecha na kucheketua.
Mashabiki wa Ali Kiba wakishow love.
Ali Kiba na mdogo wake Abdul Kiba wakizidi kuwapagawisha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live Sikukuu ya Pasaka.
Mashabiki wa Ali Kiba wakicheza staili mpya ya Chekecha Cheketua.
Shabiki wa Ali Kiba akiwa na tisheti kuonyesha kuwa yeye ni ‘Team Kiba’.
Ali Kiba akizidi kulitawala steji la kupanda na kushuka la Dar Live.
Mwanamuziki Msaga Sumu akiwarusha mashabiki wa Dar Live katika shoo ya Mwana Dar Live Sikukuu ya Pasaka.
Nyomi ikimpa shangwe Msaga Sumu.
Isha Mashauzi na kundi lake la Mashauzi Classic wakilishambulia jukwaa la Dar Live katika shoo ya Mwana Dar Live.
Isha Mashauzi akifanya yake stejini.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayefanya vizuri katika tasnia hiyo, Pamela Daffa ‘Pam D’ akiwarusha mashabiki wa Dar Live kwa songi lake kali la Nimempata.
Vijana wa Pam D wakifanya yao stejini.
Pam D akizidi kuwadatisha mashabiki.
Mshindi wa kitita cha shilingi milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Shamila Ramadhani (kushoto) akikabidhiwa hundi yake na Balozi wa promosheni hiyo, Hillary Daud ‘JayMillions’ baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo. Katikati ni mume wa mshindi huyo Abdallah Mahoka. Makabidhiano hayo yalifanyika jana wakati wa Tamasha la Mwana Dar Live, kwenye ukumbi wa Dar Live. Ili  mteja kujua kama  ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Mshindi wa milioni 10 za JayMillions, Shamila Ramadhani na mumewe wakionesha mfano wa hundi ya fedha hizo.
JayMillions akipozi na baadhi ya wadau wa Dar Live sambamba na warembo alioambatana nao baada ya kutoa mahela.