Thursday, December 25, 2014

TAMASHA LA TUONANE JANUARY (TUO8JANUARY) LAFANA MJINI MOROGORO



 Msanii mwingine wa hip hop katika anga ya Bongofleva,ambaye amekuwa akifanya vyema kwenye muziki huo,Niki wa Pili akitumbuiza katika jukwaa la wazi la Tuo8Januari lililofanyika mjini Morogoro hapo jana.



 Mmoja wa wasanii mahiri wa Hip hop,ambaye amekuwa akifanya vyema katika anga
ya muziki wa kizazi kipya,aitwaye Stamina akitumbuiza mbele ya umati wa
wakazi wa mji wa Morogoro katika tamasha la Tuo8January.


Pichani kati ni msanii Shilole akiwa sambambana madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa wakazi wa mji wa morogoro,waliojitokeza kwenye tamasha la Tuo8Januari,lililofanyika hapo jana katika viwanja vya sabasaba mkoani humo.