



![]() |
| Mmoja wa wahusika wakuu wa filamu hiyo, Bi. Rosemary Mbyalu akizungumzia namna alivyocheza uhusika katika filamu hiyo ya MAISHA YA CHUO. Katikati ni Mwenyekiti wa kundi hilo, Bw. Kyangala Gosbert na mwisho ni Nyembo Ayubu “Mmasai wa Kigoma” ambaye pia ni msimamizi wa Habari na mawasiliano wa kundi hilo.
Kikundi cha Sanaa cha Maigizo kinachoundwa na vijana zaidi ya 30 wakiwemo wanafunzi, Walimu na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kijulikanacho kama Duce Arts Group kimetambulisha rasmi filamu yao mpya ya “MAISHA YA CHUO” ambayo wanaitarajia kuizindua Ijumaa ya Juni 3, ndani ya ukumbi wa Chuo hicho kilichopo jirani na Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo Mei 30.2016, Mwenyekiti wa DUCE Arts Group, Bwana Kyangala Gosbert alieleza kuwa, filamu hiyo ambayo imechezwa na wahusika wenyewe wakiwemo
wanafunzi, wameweza kuubeba uhusika halisi wa walichokiandaa namna maisha ya Chuo yanavyokuwa na hata kupelekea matatizo kwa wanafunzi katika kufikia ndoto zao ndani ya Chuo.
“Tunawakaribisha sana siku ya tarehe 3.6.2016, kuanzia saa 12 jioni pale ukumbi wa DUCE tutaizindua rasmi filamu hii na kiingilio ni Nakala moja ya CD ya filamu ambayo itapatikana kwa shilingi 5,000. Mlangoni. Wanafunzi wa vyuo vyote pamoja na wananchi nyoote munakaribishwa” alieleza Kyangala Gosbert.
Filamu hiyo ya aina yake, inaelezea namna maisha ya Chuo wanayopambana nayo wanafunzi ikiwemo suala la mahusiano, ugumu wa masomo na hata kujiingiza katika masuala maovu ya ngono zembe, ulevi wa kupindukia pamoja na mambo mengine mabaya yanayopelekea kutofanya vizuri katika elimu yao ya Chuo.
Aidha katika uzinduzi huo wasanii mbalimbali wakiwemo wa Bongo Movie wanatarajia kupamba uzinduzi huo akiwemo msanii anayefanya vizuri kwa sasa Msanii Gabo.
|
