Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige (kushoto) akiwasili kuzindua rasmi duka la urembo la ZuRii House of Beauty linalomilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George Meru (kulia) ndani ya jengo la Dar Free Market jijini Dar es Salaam jana.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikata utepe kuzindua rasmi duka la ZuRii House of Beauty linalomilikiwa na Mwana Diaspora ambaye pia ni Blogger Jestina George Meru (anayeshuhudia tukio hilo).
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akiingia ndani ya duka hilo mara baada ya kulizindua.
Mmiliki wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George Meru akitoa maelezo ya baadhi ya bidhaa zake za urembo ambazo ni original kutoka nchini Uingereza na Marekani kwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akiangalia bidhaa za urembo wa nywele ndani ya dula la ZuRii House of Beauty lililopo ndani ya jengo la Dar Free Market linalomilikiwa na Mwana Diaspora Jestina George Meru.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikagua moja ya bidhaa za nywele ndani ya duka hilo.
Mmiliki wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George Meru akitoa ushauri na maelezo kwa baadhi ya wateja waliofika dukani kwake mara baada ya kuzinduliwa rasmi jana jijini Dar.
Raia wa kigeni nao walivutiwa na bidhaa za duka la ZuRii House of Beauty.
Mwanalibeneke Khadija Khalili akiangalia baadhi ya bidhaa ndani ya duka ZuRii House of Beauty.
Wateja wakiendelea kumiminika na kujichagulia bidhaa mbalimbali vikiwemo vibanio vya nywele vya wakubwa kwa watoto ndani ya duka ZuRii House of Beauty.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George Meru akimpa mkono wa shukrani ya kubariki uzinduzi duka hilo Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige jana jijini Dar es Salaam.

Mmiliki wa Duka la Zurii, Jestina George katika akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa duka hilo jana.

Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa duka hilo.

Jestina George kulia akizungumza na baadhi ya wanabloggers katika uzinduzi wa duka hilo jana.

Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa duka hilo.













