Tuesday, September 24, 2013

HAPPINESS WATIMANYWA NDIYE MSHINDI WA REDD'S MISS TANZANIA 2013


 Redd’s miss Tanzania 2013 mrembo Happiness Enock Watimanywa toka mkoani Dodoma akiwa na washindi wa wenzake wa shindano la Redd’s miss Tanzania mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi kwenye shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani Cituy jijini  Dar Es Salaam,Kulia ni mshindi wa Pili Latifa Mohamed toka kanda ya Temeke na kushoto ni mshindi wa tatu Clara Bayo toka kanda ya Temeke

Mkurugenzi wa masoko wa Tbl Kushilla Thomas akimkabidhi funguo za gari mshindi wa shindano la Red’s miss Tanzania 2013 mrembo Happiness Enock Watimanywa toka mkoani Dodoma  mara baaada ya kunyakua tajio hilo na kuwashinda washiriki wenzake 29  toka mikoa mbalimbali ambapo pamoja na gari lakini pia amepata kiasi cha shilingi milioni nane



SERENGETI FIESTA NDANI YA UWANJA WA KARUME MUSOMA


 Rich Mavoko akiwaimbisha mashabiki wake wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Karume mkoani Mara.
 Madansa wa msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shilole wakitumbuiza jukwaani ndani ya Uwanja wa Karume,ndani ya mji wa Musoma mkoani Mara,ambapo tamasha la serengeti fiesta 2013.
Cassim Mganga kutoka Manzabay akiwaimbisha jukwaani wakazi wa mji wa Musoma,wakati tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea ndani ya uwanja wa Karume.
 Kundi la Wanaume TMK likiongozwa na Chege na Temba wakilishambulia jukwaa la serengeti fiesta ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
 Mkali mwingine wa muziki wa Reggae kutoka kanda ya Ziwa,Jita Man akiwakumusha mashabiki wa muziki wake enzi hizo,mbele ya wakazi wa mji wa Musoma 
Godzilla kutoka maskani ya Sala sala,akishusha mistari yake live mbele ya mashabiki wake waliojitokeza kwenye tamasha la serengeti fiesta.
 Neylee akiimba jukwaani  wakati wa tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea ndani ya uwanja wa Karume,Musoma mkoani Mara.
 Kundi la Wanaume TMK Halisi likiongoza na msanii nguli Juna Nature wakilishambulia vyema jukwaa  kwa staili yao mapanga shaa shaa.
 Mwanadada Shilole akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani mbele ya maelfu ya watazamaji waliojitokeza  kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2013.
 Linah Sanga,kutoka nyumba ya vipaji THT akiimba jukwaani

 Watu kibao,kila mmoja akijaichai kivyake huku jukwaa likiwaka moto vilivyo kwa miondoko ya bandika bandua ya wasanii wanaotumbuiza. 
 Wakali wengine wanaokuja kwa kasi katika anga bongofleva-hip hop,Stamina na Youngkiller wakilishambulia jukwaa kwa kushusha mistari mikavu live.