Monday, April 4, 2016

Kamati ya Miss Tanzania yazindua msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 jijini Arusha

Miss Tanzania Arusha
Hashim Lundenga
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) akimiminiwa kinywaji cha K-Vant wakati wakiingia na wadau wa tasnia ya urembo kwenye  ukumbi wa Triple A jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 uliofanyika mwishoni mwa juma.
Hoyce Temu
Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia anasifika kwa kufanya mambo mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali kupitia kipindi chake cha ‘Mimi na Tanzania’, Hoyce Temu (katikati) akiwa na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima wakikaribishwa ukumbini na kupewa kinywaji cha K -Vant ambao walikua wadhamini wa shughuli hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha.
Lilian Kamazima
Mrembo wa Taji la Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima akakitambulishwa ukumbi kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016.

Yamoto Band
Yamoto Band ikifanya mambo yake jukwaani ndani ya ukumbi wa Triple A jijini Arusha.


No comments:

Post a Comment