Katika kujiandaa na msimu wa 201/2017, Manchester United imekodi hoteli ya kifahari ya The Lowry iliyopo katika jiji la Manchester United nchini Uingereza ambayo itakuwa inatumika kwa wachezaji kupumzika wakati wakijiandaa na michezo ya nyumbani.
Inasemekana kuwa Man United wamekodi vyumba zaidi ya kumi kwa msimu mzima ili wanapokuwa na michezo ya nyumbani katika uwanja wake wa Old Trafford waweze kufanya kambi na kuishi katika hoteli hiyo.
Hoteli hiyo ya The Lowry iliyo na hadhi ya nyota tano imekuwa maarufu kwa watu mbalimbali maarufu kupumzika katika hoteli hiyo akiwepo marehemu Muhammad Ali, Adele, Pharrell Williams, Bono, Cristiano Ronaldo na Lady Gaga.




No comments:
Post a Comment