Kampuni maarufu ya utengenezaji wa magari duniani ya Mercedes-Benz imetoa toleo jipya la gari la kifahari ambalo linatarajiwa kushindana katika soko la biashara ya magari na wapinzani wake wakubwa BMW na LEXUS.
Uamuzi wa kampuni hii maarufu duniani kutoa toleo jipya la gari la kifahari aina ya GLC43 unafuatia baada ya uhitaji wa watu na wanunuzi wa magari katika soko la biashara ya magari.
Gari hilo jipya aina ya GLC43 lililotoka hivi karibuni linafanana kiasi na toleo la gari hilo la mwaka 2015 lililofanyiwa maonyesho Shanghai nchini China.
Katika mkutano na waandishi wa habari Mwenyekiti wa kampuni ya Mercedes Bwana Tobias Moers amesema kuwa kwa uwezo na muundo mpya wa gari hilo watumiaji wa magari ya Mercedes Benz watafurahia kuendesha gari hilo.
Aidha Bw Tobias anatarajia toleo lao jipya la GLC43 litafanya vizuri katika soko la biashara ya magari likishindana moja kwa moja na BMW X4 kutoka katika kampuni ya BMW.
![]() |
| Mwenyekiti wa Mercedes Benz, Thobias Moers. |
![]() |
| Mercedes-AMG GLC43 Coupe. Mercedes-Benz |
![]() |
| BMW X4 |



No comments:
Post a Comment