Tuesday, September 13, 2016

PICHA: Uzinduzi wa mageti ya kieletroniki Uwanja wa Taifa, Dar

pix-1-9
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara yake Prof Elisante Ole Gabriel mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kukabidhiwa rasmi mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja huo Jijini Dar es Salaam.
pix-2-2
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikata utepe kuashiria kuanza kutumika rasmi kwa mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
pix-3-4
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiweka kadi  katika moja ya geti linalotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki tayari kuingia katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
pix-8
Mkurugenzi wa Kampuni ya BCEG Bw. Cheng Long Hai akizungumzia utekelezaji wa mradi wa mageti yanayotumia mfumo wa mashine za tiketi za kieletroniki uliotekelezwa na kampuni yake kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa hafla ya mkabidhiano ya mageti hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment