Tuesday, December 20, 2016

STEPHANIE DEL VALLE ATWAA TAJI LA MISS WORLD 2016, MISS KENYA ATINGA TANO BORA

miss-world-2016

Mwanamuziki na mwanamitindo kutoa nchini Puerto Rico, Stephanie del Valle Díaz ametangazwa kuwa mshindi wa taji la Miss World kwa mwaka 2016 akiwashinda wenzake 116 ambao nao walishiriki shindano hilo.
Stephanie mwenye umri wa miaka 19 kabla ya kutangazwa kuwa mshindi aliingia katika tano bora na baada ya mchojo kufanyika kwa kujibu maswali kisha majaji wakamchagua kuwa mshindi na kuchukua nafasi ya Mireia Lalaguna Royo ambaye alikuwa akilishikilia taji la Miss World kwa mwaka 2015.
Kwa upande wa Afrika Mashariki, Miss Kenya 2016, Evelyn Njambi Thungu aliwakilisha vyema kwani alifanikiwa kuingia katika tano bora akiwa pamoja na Stephanie del Valle , Yarizza Miguelina Reyes Ramirez, Natasha Mannuela na Catriona Gray
Tano Bora ya Miss World 2016
Miss Puerto Rico – Stephanie del Valle (Mshindi wa kwanza – Miss World 2016)
Miss Domican Republic – Yarizza Miguelina Reyes Ramirez (Mshindi wa pili)
Miss Indonesia – Natasha Mannuela (Mshindi wa tatu)
Miss Kenya – Evelyn Njambi Thungu
Miss Philippines – Catriona Gray

No comments:

Post a Comment